.

MAISHA YA WANAFUNZI TANZANIA 
Elimu ya Tanzania bado ina ugumu wake hasa katika suala la kujifunza vitu vigeni,wanafunzi hawa wanafundishwa kingereza lakini huelewa wao unakuwa mdogo sana katika kujifunza lugha hiyo hvyo husababisha kuwa duwaza na kumshangaa mwalimu,je tutafika? 
je wanafunzi hawa wanapata muda mzuri wa kujisomea?
Kazi wanazofanya wanafunzi wakiwa majumbani mwao huwaathiri sana katika masomo kwasababu muda mwingi wanakuwa wakijishughulisha na kazi zaidi na sio kusoma
kwa hali hii ya watoto wa mtaani watapata elimu ya kutosha na kuelimika,bado ni tatizo la taifa kukabiliana na ongezeko la watoto wa mtaani.Kama Mtanzania jaribu kufikir nakuchukua hatua.





Mazingira ni moja kati ya vitu vinavyomsaidia mwanafunzi aweze kusoma kwa uhuru.je mazingira haya mwanafunzia anaweza kusoma kwa uhuru na kuelewa anachofundishawa?

Kama inavyojulikana chakula ni msingi wa mwili wa binadamu na ukikosa chakula unaweza usifanye kazi yoyote na kuweza kufikiria,je wanafunzi wa Tanzania wanapata mlo kamili ambao utawasaidia katika kufikiria....?




Bado ni vita vikali kwenye suala la wanafunzi kufanyishwa kazi kwa muda mrefu.
Hapa wanafunzi wanabebeshwa madawati wakati huohuo vipindi vya masomo vinaendelea je watasoma saa ngapi kama wanaendelea kufanya kazi hizo na wakifeli mitihani nani alaumiwe?Chukua atua kuwa mkombozi wa elimu ya Tanzania.



Wazazi nyumbani pia huchangia suala la kufeli kwa wanafunzi kwasababu ya kazi nyingi wanazowapa wakati wkiwa nyumbani n akusababisha wakose muda wa kujisomea.
Tubadilike na kuchukua hatua ili watoto wetu na wadogo zetu wapate elimu bora na sio bora elimu....!